KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi
karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26),
mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba
ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina.
Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika
Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara
yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.
Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama
ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu
baada ya wanahabari kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu
lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.
Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:
“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana
wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye
aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.
“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu
akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi
saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili
nije kupata pesa.”
Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa
ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa
ameshikilia upande wa khanga.
Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa
mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali
wa kamera walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai
hayawahusu .
No comments:
Post a Comment