Na Issa Mnally
DUNIANI kuna mambo jamani! Usiku wa
kuamkia juzi ulikuwa mbaya kwa mke wa mtu, Rukia Issa au mama Sabrina
baada ya mumewe, Shukuru Nia kumfumania gesti na mwanamme mwingine huku
yeye akiwa na kichanga cha miezi miwili na nusu, Risasi Mchanganyiko
linakupa vitu.
Rukia ambaye ni mkazi wa Goba, Wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam alifumaniwa katika gesti moja (jina
tunalo) iliyopo Mbagala, Dar akiwa na mwanamme aliyefahamika kwa jina la
Ally Said ambaye pia ni mkazi wa Goba.
MAELEZO YA AWALI
Ilielezwa kuwa, siku ya tukio Rukia
akiwa na kichanga chake mgongoni alimuaga mumewe kwamba anakwenda
kwenye msiba Kongowe wilayani Temeke, Dar ambako angelala mpaka siku ya
pili yake, yaani Jumanne.
Mume alimruhusu mkewe huyo huku akimwagiza akawape pole wafiwa wote.
SHAKA NAMBA MOJA
Mnyetishaji wetu akasema mke alipondoka
na mume alitoka nyumbani kwenda kununua mahitaji f’lani dukani, kwa
mbali alimwona mke wake huyo amesimama akizungumza na mwanamme mmoja
ambaye amekuwa akimshuku anatembea naye.
MUME AWAWEKA ‘WAPELELEZI’ MSIBANI
Kufutia tukio hilo la mkewe kusimama na
‘mwizi’ wake, mwanamme huyo aliamua kumpigia simu nduguye mmoja
aliyekuwa msibani na kumweleza hisia zake kuhusu safari ya mkewe baada
ya kumwona amesimama na jamaa, akamwambia akifika tu kwenye msiba
amfuatilie kwa undani nyendo zake.
MKE, KICHANGA MGONGONI ATINGA MSIBANI
Habari zinadai kuwa, safari ya mama
Sabrina ilimfikisha msibani Kongowe kama alivyomuaga mumewe na
alishiriki shughuli zote ambazo alipangiwa huku uso wake ukionesha
majonzi ya msiba huo.
Chanzo chetu kikazidi kueleza kuwa ilipofika majira ya saa tano usiku, akakibeba kichanga chake na kuondoka bila kuaga mtu.
‘SHUSHU’ AMFUATA KWA NYUMA
Baada ya mama Sabrina kuondoka tu, hata
hajafika umbali wa uwanja wa mpira, kijana mmoja akatumwa na mtu
aliyepewa jukumu la kumfuatilia nyendo mwanamke huyo, akaambiwa atembee
nyuma yake hadi atakapoishia.
Mtoa taarifa anasema ni ndani ya dakika
kama kumi na tano tu, kijana huyo alirejea na ujumbe kuwa, mama Sabrina
aliingia gesti na mwanamme, mrefu kidogo, amevaa sendozi, suruali ya
kadeti na T-shirt nyekundu yenye michirizi ya rangi nyeupe na chata ya
Adidas upande wa kushoto wa kifua.
MUMEWE APIGIWA SIMU
Kijana akaulizwa: Mtoto je?
Kijana: Ameingia naye, tena kambeba mgongoni.
Watu waliokuwa msibani hapo wakaulizana
nani ana simu yenye muda wa maongezi wa kutosha? Akajitokeza mmoja
ambapo simu yake ikatumika kumpigia mume wa mwanamke huyo na kumpasha
kila kitu.
Mume baada ya kupata taarifa hizo
zinazoweza kumpa mtu ugonjwa wa moyo ghafla, alifanya mawasiliano na
baadhi ya ndugu wengine ikiwa ni pamoja na kumtwangia simu mpigapicha
wetu.
Ilikuwa saa 8:34 usiku, tukio lipo
Mbagala, mpigapicha wetu yupo Kijitonyama, Kinondoni. Ilibidi apande
pikipiki yake iendayo kasi kuliko nyingine katika teknolojia ya kisasa.
Ndani ya nusu saa, mpigapicha watu, mume
wa mwanamke huyo, ndugu wengine na kijana aliyetumwa kufuatilia
walikusanyika nje ya gesti hiyo na kupanga mbinu ya namna ya kuvamia
chumbani ambapo waliipata.
Baada ya kuvamia, wote walipigwa butwaa
kufuatia kumkuta mama Sabrina na jamaa yake wakiwa ‘vibaya’ huku
kichanga kikiwa pembeni kimelalishwa chali tena kikiwa macho, maskini
malaika wa Mungu.
MUME APAGAWA, ASEMA YOTE
Baada ya kuona kwa macho yake tukio hilo
ambalo halitatoka kirahisi kwenye kumbukumbu zake kichwani, baba
Sabrina alipagawa. Akamgeukia mpigapicha wetu:
“Ndugu mwandishi, siku moja nilikutana
na huyu bwana, ni jirani yangu kule Goba, kwa kuwa nilishasikia
anatembea na mke wangu nikamwomba aachane naye.
“Cha ajabu alinijibu kwa ujeuri kuwa
niachane na yeye kwa vile hatembei na mke wangu, mbaya zaidi akanisukuma
nikaanguka, nikajizoazoa pale na kuondoka zangu, niliumia sana.
Akamgeukia mkewe: Kwanza inawezekana
huyu mtoto si wangu, umemleta hapa gesti kwa baba yake ili umtambulishe.
Hata huyu mtoto nakukabidhi mimi si wa kwangu, haiwezekani arobaini
yake tangu azaliwe imepita juzijuzi tu, hata mimi sijakuingilia kwa
sababu una mtoto mchanga leo unakuja kufanya upuuzi wako huku, hapana
huyu si mwanangu.
NDUGU WASHINDWA CHA KUSEMA, SIKIA UTETEZI WA MKE
Ndugu na jamaa walishindwa kuongea
chochote kutokana na mshtuko lakini mama Sabrina kwa upande wake
alijaribu kujitetea kuwa, hamu ya mapenzi ndiyo ilimshawishi kufanya
hivyo.
WAPELEKWA POLISI
Mwisho wa sakata hilo, wawili hao
(mwanamke akiwa na mtoto wake mgongoni) walipelekwa katika Kituo cha
Polisi cha Oysterbay, Dar kwa ajili ya hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment