STAA wa sinema na Bongo Fleva, Baby
Madaha amenaswa live akiingia na kula bata hotelini akiwa na mwanaume
aliyetajwa kwa jina la Joe Kariuki.
Tukio hilo lililopigwa chabo na
shushushu wetu lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya usiku mnene katika
Hoteli ya De France iliyopo Sinza, Dar ambapo Madaha alionekana akiwa
amejiachia vya kutosha kwa mwanaume huyo
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti
hili lilizungumza na Madaha ambaye alikiri kuwa na mwanaume huyo
hotelini hapo huku akidai ni meneja wake.
“Joe (Kariuki) ni meneja wangu wa
Kampuni ya Candy n’ Candy Records ya Nairobi, Kenya ndiye anayesimamia
kazi zangu na tayari nimeachia ngoma moja inayo-hit ya Summer Holiday,”
alijitetea Madaha.
No comments:
Post a Comment