Jumamosi takriban saa tano unusu
asubuhi, genge la kigaidi linaloshukiwa kuwa la Al Shabaab lilipata
kungia katika eneo la kibiashara la Westgate wakiwa kwenye magari ya
kibinafsi.
Kundi hilo la takriban watu 10-15
liliweza kuingia kupitia lango kuu la jumba hilo huku lingine likiingia
kutoka eneo la kuegeshea magari lililoko paani.
Katika lango kuu walianza kwa kumuua
mkurugenzi wa kampuni ya usalama inayolinda eneo hilo kabla ya kuelekea
paani ambapo ulikuwa na hafla iliyoandaliwa na idhaa ya East FM.
Wale walioingilia lango kuu
wakafululiza hadi duka la Nakumatt lililoko katika jengo hilo na ni
hapa ambapo mauaji ya Wakenya wasiokuwa na hatia yoyote yalipoendelezwa
zaidi.
Milio ya risasi ikasheheni angani.
Huku haya yakijiri tayari maafisa wa
polisi walikuwa wamepata habari hizo na vikosi mbali mbali vikakita
kambi na kulizingira eneo hilo, magharibi, mashariki, kusini na hadi
angani.
Shughuli ya uokozi ikaanza ili
kufanikiwa kuwashikilia mateka kwa siku tatu mtawalia huku vikosi vya
usalama vinajua ina maana kuwa magaidi hawa walikuwa wamejihami
vilivyo.
Na je ni akina nani hawa ?
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa,
washukiwa hawa ni watu wa tabaka na mataifa mbali mbali wakiwemo
wafuatao wanaodaiwa kushiriki kwenye shambulizi hilo:
1. Sayd Nuh – 25 – Kismayu
2. Ismael Galed – 23 – Finland
3. Mustafa Noordiin – 24 – Marekani
4. Abdifatah Osman- 24 – Marekani
5. Kassim Musa – 22 – Garissa
6. Mohammed Badr – 24 – Syria
Aidha waziri wa masuala ya ndani na
usalama Joseph Ole Lenku amefutilia mbali madai kuwa kiongozi wa kundi
hilo ni mwanamke akishikilia kwamba ni wanaume waliovalia mavazi ya
kike.
Kufikia sasa vikosi vya kenya vya
usalama vimechukua usukani wa orofa zote za jengo hilo, na kulingana na
Lenku ni kuwa magaidi wangali wamejificha, japo wawili tayari
wameuawa.