Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na
msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya
kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
Katika
tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini
Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa
amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika
maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini
tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa
wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya
saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika
mapajani.
Shushushu
wetu aliwapiga chabo ‘wakifanya yao’ hadi Diamond alipokwenda stejini
na kuangusha bonge la shoo huku akimwacha Linah mpweke.
Kwa mujibu
wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’
anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
Mwanahabari wetu alipomuuliza Linah kuhusu ishu hiyo, alifunguka: “Weweee…hakuna ni mapozi tu na wala usiandike hiyo habari.”
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi
kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo
kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.
No comments:
Post a Comment