Mwanzoni mwa juma hili,nilitembelea shule moja ya wasichana nikiwa na shida ndogo ya kiofisi hapo.
Jina la shule naomba nilihifadhi sina taaluma ya uandishi wa habari,nisikiuke misingi yake.
...
Nilipofika ofisini nilikaribishwa staff ya walimu,nikaambiwa
nisubiri.Hapo ndipo niliduwaa kumuona mwalimu mmoja wa kike akiingia
ofisini na mtoto wa kike,kidato cha tatu huku akiandamwa na fimbo za
mgongoni.
...
Tatizo lilikuwa kwamba,,yule binti alikuwa amekamatwa jumapili yake(siku iyo ilikuwa jumatatu)
Akiwa amelala na wanaume wawili wakati wenzake wameruhusiwa kwenda
nyumba ya ibaada.Shule yenyewe ina taratibu ya kuwaruhusu wanafunzi
kuhudhuria ibaada nje ya shule ambapo ni mwendo wa dk 25 ivi kwa
miguu... Mwanafunzi huyu alikiri kulala na wanaume hao wawili na
alipoulizwa
aliwafaham vipi,alisema alitumia simu ambayo pamoja na shule kuzuia bado
aliiweka kwenye taiti,,ikiwa na vibration.Aliweka wazi kuwa matroni
hata akague vipi hawezi kuwakamata wote maana wanafunzi wengi wana simu.
...
Alipoulizwa anapaje ujasiri wa kulala na wanaume wawili,huku akilia
anasema alikubaliana na mmoja,akaongezeka wa pili,,hivyo asingeweza
kuwazuia.
...
Tukio hili ambalo bado linaendelea kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo
wahusika kutafutwa,,lilinifanya niondoke na maswali mengi kichwani.Je
tuwafiche wapi? Je malezi gani tuyatumie? Je wazazi walio nyumbani
wanajua watoto wao wanamiliki simu? Je imefika mahali,somo la Mahusiano
Urafiki Mawasiliano na Mapenzi liwekwe shuleni? Je hawa ndo wake wema na
waume wema wa kesho?
Iliniuma,,jamani tusitafute wa kulaumu bali nini kinaweza kuleta usalama.
No comments:
Post a Comment