Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu
Mchungaji wa nchini Afrika Kusini amewafanya waumini wake wale majani kama mbuzi ‘eti’ kuwa karibu na Mungu.
Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake
Kwa maelekezo ya Pastor Lesego Daniel
wa Rabboni Centre Ministries, mamia ya wafuasi wake walijimwaga kwenye
uwanja nje ya kanisa lake kula majani huko Garankuwa, Kaskazini mwa
Pretoria baada ya kuambiwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa karibu na
Mungu.
Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao
Mbinu hiyo yenye utata imekosolewa na
watu wengi huku yeye akisema kuwa binadamu wanaweza kula chochote na
wasidhurike. “Ndio tunakula majani na tunajivunia sababu inaonesha kuwa
kwa nguvu ya Mungu, tunaweza kufanya lolote,” Rosemary Phetha
aliliambia gazeti la Afrika Kusini la Times Live.
Doreen Kgatle, 27, alipata kiharusi
miaka miwili iliyopita anasema: Sikuweza kutembea lakini baada ya kula
majani kama mchungaji alivyoagiza, nilianza kupata nguvu na saa moja
baadaye niliweza kutembea tena.”
Picha zinazoonesha waumini mbalimbali wakila majani huku mchungaji huyu akiwakanyaga zimeleta mjadala mkubwa.
Matokeo baada ya kula majani, kuumbwa tumbo na kutapika
Times Live limeandika kuwa kwenye misa
hiyo ya watu takriban 1,000 Daniel alisikika akisema ‘lala’ na watu
sita wakalala usingizi. Aliwaagiza watu wengine kuwapiga vibao na
kuwatikisa lakini watu hao walienda kulala bila kujitambua hadi pale
alipowaagiza waamke.
‘Unaweza kuwaacha hivi kwa miezi sita. Naipenda hii. Sipendi kuboreka. Unaweza hata kuwafanya polisi wasinzie pindi wanapokuja kukukamata,” alisema.
No comments:
Post a Comment