Sunday, 1 December 2013
It real sad R.I.P Paul Walker,this information we get from Paul Walker facebook account
Marekani. Mwigizaji wa Fast & Furious, Paul Walker amefariki dunia hivi punde nchini Marekani baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo kukosa ‘control’ na kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani.
Nyota huyo wa kuigiza mwenye umri wa miaka 40 alikuwa abiria kwenye gari ya kisasa na ajali hiyo ilitokea katika eneo la Santa Clarita.
Idara ya usalama ya nchini humo imedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba watu wawili wamefariki dunia kwenye ajali hiyo.
Wawakilishi wa mwingizaji huyo wamethibitisha kwamba Paul Walker ni mmoja wa watu wawili waliofariki mchana wa LEO nchini Marekani.
“Ni kweli, tunapenda kuthibitisha kwamba mwigizaji Paul Walker amefariki dunia leo katika ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa akienda kuudhuria kuchangia mfuko wa Reach Out Worldwide.
“Alikuwa abiria kwenye gari ya rafiki yake na wote wamepoteza maisha leo,”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment