Tuesday, 31 December 2013

NDOA YA RAIS BARACK OBAMA NA MICHELLE YAINGIA TIMBWILI, HIKI NDICHO KISA KINACHOONEKANA KUITIFUA NDOA YAO. Read more: http://www.aalkanes.blogspot.com/2013/12/ndoa-ya-rais-barack-obama-na-michelle.html#ixzz2pDfjCJJO


NDOA YA RAIS BARACK OBAMA NA MICHELLE YAINGIA TIMBWILI, HIKI NDICHO KISA KINACHOONEKANA KUITIFUA NDOA YAO.  


Michelle akiteta jambo na Helle.
  
WASHINGTON, Marekani.
NDOA ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle haitaweza kuvunjika kwa sasa kwa vile mke huyo mrembo atatakiwa kuendelea kuishi katika Ikulu ya White House hadi mumewe atakapomaliza muhula wake wa pili wa uongozi mwaka 2016.
Obama akiwa 'busy' na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa mazishi ya Mandela Afrika Kusini. Kulia ni mkewe Michelle. Obama akimbusu Helle Thorning-Schmidt mbele ya mkewe. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Michelle, mama wa watoto wawili, Sasha na Malia, hata kama ataachika atalazimika kuendelea kubakia ikulu kwa ajili ya mahitaji ya kuwa pamoja na mumewe katika hafla za kiserikali zinazohitaji uwepo wa mke. Hiyo ndiyo sera ya Ikulu ya Marekani.

Akifurahia jambo wakati mkewe kanuna. 
Juzi, Gazeti la The Nation la Marekani liliripoti kuparaganyika kwa ndoa hiyo iliyowahi kutajwa kama ndiyo bora zaidi duniani, kwa kile kilichoelezwa kuwa kuchukia kwa Michelle baada ya kumwona mumewe akishoboka na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa shughuli za kumuaga rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela ‘Madiba’.
Obama akipiga picha na Helle. Vyanzo katika mitandao mbalimbali vilisema ndoa hiyo ilikuwa inawaka moto kwa muda mrefu na kwamba hata kabla Michelle hajaanza kuishi katika jengo la peke yake katika viwanja hivyo vya ikulu, walikuwa wakilala ‘mzungu wa nne’.

Helle akimuonyesha kitu Obama. Mwaka 2012, uvumi ulisambaa kwa kasi duniani ukielezea kutengana kwa watu hao wawili maarufu zaidi, hali iliyosababisha Ikulu ya Marekani kukanusha taarifa hizo.
Michelle baada ya kuamua kukaa kati yao.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ikulu, Obama wala Michelle juu ya madai ya kutengana kwao.

Sunday, 1 December 2013

It real sad R.I.P Paul Walker,this information we get from Paul Walker facebook account


Marekani. Mwigizaji wa Fast & Furious, Paul Walker amefariki dunia hivi punde nchini Marekani baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo kukosa ‘control’ na kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani.

Nyota huyo wa kuigiza mwenye umri wa miaka 40 alikuwa abiria kwenye gari ya kisasa na ajali hiyo ilitokea katika eneo la Santa Clarita.

Idara ya usalama ya nchini humo imedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba watu wawili wamefariki dunia kwenye ajali hiyo.

Wawakilishi wa mwingizaji huyo wamethibitisha kwamba Paul Walker ni mmoja wa watu wawili waliofariki mchana wa LEO nchini Marekani.




“Ni kweli, tunapenda kuthibitisha kwamba mwigizaji Paul Walker  amefariki dunia leo katika ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa akienda kuudhuria kuchangia mfuko wa  Reach Out Worldwide.



“Alikuwa abiria kwenye gari ya rafiki yake na wote wamepoteza maisha leo,”