MWANADADA anayeendesha maisha yake
kwa kuPkupitia filamu za Bongo, Wastara Juma ameumia mguu baada ya
kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na paparazi wetu siku
chache baada ya kurudi Bongo, Wastara alisema aliumia wakati akifanya
mazoezi ya mguu mpya aliowekewa ambapo kwa sasa anaendelea kuuguza
jeraha hilo na amerudi mara moja kwa ajili ya Sikukuu ya Idd,
ikimalizika atarejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Nimeshindwa kula sikukuu mbali na
watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa
sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi na
sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa
ajili ya matibabu,” alisema Wastara.
No comments:
Post a Comment