Angalia baadhi ya picha jinsi moto ulivyowaka Serengeti Fiesta Dar es salaam Jana katika Viwanja vya Leaders
Sunday, 27 October 2013
NOMA SANA.....! ANGALIA PICHA ZA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 VIWANJA VYA LEADERS USIKU WA JANA
Angalia baadhi ya picha jinsi moto ulivyowaka Serengeti Fiesta Dar es salaam Jana katika Viwanja vya Leaders
Saturday, 26 October 2013
POLISI WAMKAMATA NEY WAMITEGO NA KUMSWEKA SERO !
VIDEO YAKE NEY WAMITEGO "SALAAM ZAO" YAMSABABISHA NEY KUKAA SERO,
POLISI WATANDA SEHEMU YA TUKIO WAKIHOJI KIBALI KWA NEY KUTUMIA SARE ZAO,
WAMKAMATA NA KUMSWEKA SERO URAFIKI POLICE POST,
PICHA ZIMA LILIKUWA JANA.
Wednesday, 23 October 2013
AIBU. TENA SI NDOGO..!! MUME NA MKE WA MTU WANASWA LIVE GESTI WAKINGONOKA BUGURUNI-SOKONI..
Live: Mume wa mtu, Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema baada ya kunaswa gesti saa 7 usiku.
Wawili hao
walinaswa hivi karibuni kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue
Roze maeneo ya Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.
Habari
zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya
leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu
hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa
baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono
ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini, vijana wa OFM walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!

Wakati huohuo,
kijana mwingine wa OFM aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya baa
hiyo ili kupeleleza bei zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei kwa
kuwa alikuwa na changudoa kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na wengine
waliokuwa wanatoka nje ya eneo hilo.
TAARIFA POLISI
Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.

Ilipotimia
usiku wa manane, ndipo zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu
kuingia ndani ya baa hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya
gesti.
Akiwa ndani,
paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani
huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi
kufanyika tu.
KAZI IKAANZA
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Katika
pekuapekua hiyo ndipo mume huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa
mtu huku wote wakiomba msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo
haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
“Chondechonde
mimi nina ndoa na familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu.
Naombeni tuyamalize kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa
polisi, utetezi ambao haukumsaidia.
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
“Hatujazitumia
sisi hizi, tumezikuta humuhumu chumbani. Lakini nawaombeni sana,
msinipeleke polisi nina ndoa yangu. Naombeni mnisamehe kwa sababu mume
wangu atanirarua. Ninyi wenyewe mnajua ndoa ilivyo ngumu, tafadhali
naomba mnisitiri,” alisikika mwanamke huyo.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.
Mbali
na hao, oparesheni hiyo pia ilimtia nguvuni meneja wa eneo hilo,
Emmanuel Mpinge, ambao wote kwa pamoja walifikishwa kituoni na
kufunguliwa kesi yenye namba BUG/RB/13114/2013 - KUFANYA VITENDO VYA
UMALAYA 19/10/2013.
Sunday, 20 October 2013
HIKI NDICHO KILICHOTOKEA JUU YA MWANAMKE ALIYETOKA KUJIFUNGUA NA KUJIRUSHA KUTOKA GOROFANI NA KUFARIKI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI
KUNA simulizi ya majonzi nyuma ya kifo cha mwanamke Lewina Kinemo (38)
aliyedaiwa kujirusha ghorofani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), Dar es Salaam ambako alikwenda kujifungua.
Lewina alifariki dunia Jumanne iliyopita saa tano na dakika arobaini alipokuwa anatoka kumnyonyesha mwanaye aliyezaliwa wiki moja nyuma.
MWANAMKE ALIYEKUWA NA MAREHEMU
Kwa mujibu wa mwanamke aliyekuwa na Lewina (jina halikupatikana mara moja) muda mfupi kabla ya kifo, marehemu alifanya mambo yenye viashiria vya kifo chake na hajui nini kilimtokea.
Alisema: “Unajua baada ya kujifungua, watoto waliopatikana na matatizo walitengwa kwenye chumba maalum ghorofa ya pili, sisi wazazi tukawa chini.
“Sasa tulikuwa tunatakiwa kupanda ghorofani kwenda kuwanyonyesha watoto kila baada ya saa tatu kupita. Ili kwenda, ililazimika kupanda lifti lakini kwa sababu yeye alijifungua kwa upasuaji, daktari alimshauri asiwe anapanda lifti.
“Tulipanda mara kadhaa, lakini safari ya mwisho ambayo marehemu alikutana na kifo chake, baada ya kumaliza kumnyonyesha mwanaye, alimshika akamwangalia sana kisha akasema maskini mwanangu sijui utabaki na nani?
“Mimi sikutilia maanani kauli yake, kumbe alijua atakufa.
“Kuna wakati tukiwa wodini alisema yeye ana duka la kushona nguo, akawa anahoji siku atakapokuwa hayupo nani atasimamia biashara zake kwani mumewe naye ni mfanyabiashara kwa hiyo yupo bize.
“Nilimuuliza anataka kwenda wapi hadi anasema hivyo, akajibu amewaza tu. Kumbe mawazo yake ni kama alijua dakika chache mbele ataiaga dunia.
“Sisi tuliokuwa tunatumia lifti tulipofika vyumbani mwetu tulijua yupo nyuma yetu. Kishindo kikubwa cha kitu kizito kuanguka ndicho kilichotushtua lakini hatukutoka nje.
“Baadaye ndiyo tukaletewa habari kwamba mwenzetu mama kichanga alianguka na kufa. Tulishtuka sana, tulilia kwani marehemu alikuwa mchangamfu kwa kila mtu ingawa siku ya kifo kama alipooza au kukosa raha. Kuna mwenzetu mmoja alimuuliza mbona leo huna raha, akasema anawaza maisha yake ya mbele,” alisema mwanamke huyo.
ALIJIRUSHA AU ALIANGUKA?

![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjNFjc4CV7zJojfll7Gr5X7cssLUpxxIAbqzL97sYZrmGsQ4GYAy1NDvdt43akv7BoExryVNevDTH7LN_n1-Y3TMvq2D5RVZnS2-RGDfIALpYCh6XUMJyaUgMekNFDKkwJhIf8OJM-hGOZ8/s640/simulizi.jpg)
“Hatujui. Hata manesi wenyewe walisema walimkuta amekufa chini, kwa hiyo hawajui kama alianguka au alijirusha kwa kuwa hakuna aliyemuona.”
MUME WA MAREHEMU NAYE
Akizungumza kwa uchungu kwenye msiba wa mkewe, Sinza - Mori jijini Dar, mume wa marehemu Lewina aitwaye Mashaka Mkude alisema:
“Kifo cha mke wangu mimi najua kilitokana na uchovu wa kupanda na kushuka kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya pili kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto.
“Mke wangu akiwa mjamzito alifika Muhimbili akiwa mzima wa afya, akajifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji.
“Baada ya kujifungua, hali ya kichanga ikiwa si nzuri kiafya, alionekana ana manjano, yaani hali ya kubadilikabadilika na akalazimika kutengwa yeye na mtoto wake.
“Kutoka na hali hiyo mke wangu alishauriwa na daktari awe anakwenda kumnyonyesha mtoto kila baada ya saa tatu.
“Ilikuwa usiku wa saa sita kasoro, siku ya Jumanne, yeye na wenzake walipoamka kwenda kunyonyesha inadaiwa hakupanda lifti kama wenzake.
“Wakati wa kurudi inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na mwenzake wakati wa kushuka, akashauriwa atumie lifti lakini alikataa.
“Baada ya muda mfupi wenzake walisikia kishindo kikubwa kumbe ni mke wangu alianguka kutoka juu na kufariki dunia palepale.
“Nina imani mke wangu alikuwa katika utaratibu wa kutimiza ushauri wa dakrari wake hali iliyompata ilitokana na uchovu wa kupanda ngazi na kushuka,” alisema mwanaume huyo.
Mashaka alikanusha vikali kuwa mke wake alijirusha na kumsababishia kifo, akisema marehemu hakuwa na tatizo lolote la kifamilia wala kiafya.
AZIKWA, KICHANGA BADO HOSPITALI
Habari zinasema kichanga hicho walichokipa jina la Biligita Mashaka kinaendelea vizuri katika uangalizi maalum hospitalini hapo ambapo kinawaliza wengi kutokana na masaibu yaliyotokea.
Marehemu alizikwa Ijumaa ya wiki iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
KAMANDA WA POLISI ILALA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema marehemu alikutwa chini amekufa baada ya kuanguka kutoka kwenye ngazi za ghorofani.
Subscribe to:
Posts (Atom)